December 9, 2017




Kocha wa Simba, Joseph Omog amefurahishwa na mabao iliyonayo timu yake katika Ligi Kuu Bara lakini ameagiza wachezaji wake wafunge mabao mengi zaidi ili njia ya ubingwa iwe rahisi.

Omog anataka mabao hayo yawape wepesi wa kutwaa ubingwa kama ilivyofanya Yanga msimu uliopita ambapo ilitwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.

Msimu uliopita, Yanga na Simba zilimaliza ligi kuu zikiwa na pointi 68, lakini Yanga ikawa bingwa kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga ilifunga mabao 57 na kufungwa 14, huku Simba ikifunga mabao 50 na kufungwa 17.

Hivi sasa, Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 23 sawa na Azam FC, huku ikifunga mabao 22 ambayo ni mengi zaidi kuliko timu nyingine.

Inayofuatia kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga ni Yanga iliyo na mabao 17.

Akizungumza kutoka Cameroon, Omog amesema kitu
cha kwanza anachokifanyia kazi msimu huu ni kuhakikisha wanakuwa na idadi kubwa ya mabao kwani tayari wamejifunza na makosa.

“Mpaka sasa ukiangalia tumefunga mabao mengi kuliko timu nyingine na hilo ndilo nilikuwa nalihitaji liwepo kwa msimu huu baada ya msimu uliopita kukwama sehemu ndogo tu katika kuchukua ubingwa.

“Nimewapa mbinu mbalimbali washambuliaji na kuwaagiza wafunge mabao mengi ili iwe rahisi katika kutubeba kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Omog.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic