December 12, 2017



Kampuni ya kubashiri michezo ya kubashiri matokeo ya SportPesa Tanzania imeingia makubaliano ya kudhamini mashindano ya michezo ya wanavyuo ijulikanayo kama SportPesa Tusa Games.

Makubaliano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Peninsula House jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Afisa Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika Desemba 14 hadi 20 mwezi huo, mwaka huu Mkoani Dodoma.

Msuya alisema, katika mashindano hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ambayo iyafunguliwa rasmi keshokutwa Ijumaa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma.

Aidha, aliitaja michezo itakayoshindaniwa ni soka, netiboli, vollyboli, kriketi, karata, drafti, tenisi na swimming pool.

“Kwa miaka mingi tumeona nchi za wenzetu zilizoendelea zikinufaika na vipaji kutoka kwenye mashindano ya vyuo vikuu ambavyo vimeweza kung’aa hadi kwenye ngazi ya timu ya taifa.

“Kwa hiyo kama SportPesa kama wadau wa maendeleo ya soka nchini, tumeona ni muhimu kudhamini mashindano haya ili tuweze kuvipa nafasi vipaji vilivyojificha kwenye vitabu viweze kuibuka ili kuua hile dhana kuwa wasomi hawana vipaji vya ziada,” alisema Msuya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic