Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga inaendelea kujifua kuhakikisha inatetea taji lake la Ligi Kuu Bara, sasa ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.
Yanga haijawa na mwendo mzuri sana lakini wachezaji wake wameonekana kupania kubadili mambo wakiwa na juhudi kubwa mazoezini.
MSIMU HUU KWA YANGA NI MZURI::
ReplyDeleteKatika misimu zaidi ya mitatu sasa...Yanga ilianza kwa kusuasua angalau ilichukua ubingwa..Msimu uliopita kumbukumbu zinaonesha takribani mechi zake tatu za mwanzo walipokea kipigo. Kufika raundi ya tano had sita Yanga ilikuwa inashika nafasi ya Kumi na mbili (12).
Mwaka huu Yanga haijaanza kwa kusuasua angalau ina wachezaji wengi tegemeo ni majeruhi. Kinachofanya ionekane imesuasua ni utimamu wa ligi ya Safari hii. Timu nyingi zimejiandaa vizuri na naamini Timu itakayochukua ubingwa itafanya kazi kubwa.
Mwaka ambao timu nyingi hazijapitana sana ni mwaka huu...ukiangalia timu zilizo juu zinapitana kwa wastani wa pointi mbili ambazo yoyote anaweza kufanya mabadiliko.Timu ambayo imepunguza wachezaji wenye gharama kubwa (Azam FC) ndio timu iliyo imara kwa kutumia kikosi chake kwani hadi sasa kina pointi 23 nyumba ya Simba yenye pointi 23 lakin wamepishana kwa wastani wa magoli. Yanga SC bado inamatumaini ya kufanya vizuri kwa kuwa wachezaji wake majeruhi wameanza kujifua. Kwahyo tuamini mabadiliko kwenye awamu hii inayofata baada ya mapumziko ya CECAFA.
Ndugu zangu Singida wao wanashika nafasi ya nne (4)..hawapo vibaya wanakuja. Ndugu zangu Mtibwa wao ni kama gari linalokosa muelekeo. Mtibwa ina historia ya kuongoza ligi kwa takribani mechi nne au tano..wakati mwingine wanafanya vizuri msimu wa kwanza ila ikifika msimu wa pili wanaanza kupotea.
Huwa sijuagi mbinu mkakakti wao ni kubaki ligi kuu au nao kuchukua ubingwa. Mara nyingi huwa inashuka kwa kiwango kikubwa kwenye msimamo wa ligi angalau huwa inamenteini kutoporomoka zaidi...wajitazame upya.
NASHUKURU KWA KUCHANGIA