December 22, 2017



Simba imevuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya Green Worriors inashiriki Ligi Daraja la Pili.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, iliisha kwa sare ya mabao 1-1 kwa dakika 90.

Baada ya hapo iliamualiwa kwa mikwaju ya penalti na wachezaji watatu wa Simba, Muzamiru Yassin, Hussein Zimbwe ’Tshabalala’ na Jonas Mkude walikosa penalti zao.


Kipa Aishi Manula wa Simba na Shabani Dihile walijipangua mikwaju ya penalti

3 COMMENTS:

  1. Duh ningekuwa OMOG ....ningeshajiuzulu ukocha kabla ya hata penalti kupigwa.Klabu imeshaingia kwenye uwekazaji hivyo MO DEWJI vunja benchi la ufundi...Turudishieni Cirkovic au Kuponovic.

    ReplyDelete
  2. Hapana shaka tatizo la simba halina tofauti la Kilimanjaro stars. Kutojielewa au kujitambua kwa wachezaji wa kibongo hasa wale wanaochezea simba na yanga ni tatizo .

    ReplyDelete
  3. Hahahahaaaaa hii ndiyo soka ya Bongo. Daraja la pili!!! Simba nje!!! Basi tena mashindano hayana tena Bingwa Mtetezi. Pole yako mtani. Umekamiwa kweli!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic