December 16, 2017



Huku dirisha dogo la usajili likifungwa jana saa saa 6:00 usiku, Yanga imefunga na wachezaji wawili, mshambuliaji na beki mmoja wa kati.

Wachezaji hao waliosajiliwa na Yanga ni beki raia wa DR Congo, Fistoni Kayembe na mshambuliaji Yohana Nkomola aliyekuwa kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoshiriki Kombe la Chalenji.

Yanga imewasajili nyota hao mkataba wa miaka miwili kila mmoja kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani ambapo wataanza na St Louis ya Shelisheli.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema wao wanafanya usajili kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha wao George Lwandamina.

Mkwasa alisema, hawana mpango wa kuongeza mchezaji mwingine katika kipindi hiki baada ya usajili wa Nkomola na Kayemba kumalizika, kwani ndiyo mapendekezo ya Lwandamina.

Alisema walikuwa na mpango wa kuwasajili washambuliaji wengine wawili kutoka Sierra Leone na Benin ambao waliwapelekea mwaliko kwa ajili ya majaribio ili wachukue nafasi za majeruhi, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

“Tunafunga usajili wa dirisha dogo na hawa wachezaji wawili ambao ni beki Kayembe na straika Nkomola, hatuongezi mchezaji mwingine.


“Tulitaka kusajili mastraika wawili lakini tumesitisha mpango huo kutokana na hali za majeruhi Ngoma na Tambwe kuwa nzuri, hivyo tumeachana na usajili mwingine,” alisema Mkwasa.

1 COMMENTS:

  1. Nafikir fedha baba ndiyotatizo lililositisha usajili Mpya Wa kutisha,na ndiyo hofu ya kumtema Ngoma pia.Tuweke hadharani tusizungukezunguke,itatugharimu kesho.kama mji una njaa pigs kelele wenzio wake wafanye msaada.hivi unawezaje kuwamwaga strainers watano ukasajili mmoja.?Ni kazi nzito jamani tunauendea Moira Wa majuu,jitihada ifanyike kuandaa kikosi bora jamani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic