December 25, 2017



Beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani, hivi sasa yupo kwao Mwanza alipoenda kupumzika akiuguza majeraha ya enka na anatarajiwa kuanza mazoezi Desemba 28, mwaka huu ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Yondani ambaye aliumia akiwa na kikosi cha Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya, kwa takriban wiki mbili sasa yupo Mwanza.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, maendeleo ya Yondani hivi sasa ni mazuri kutokana na kupatiwa matibabu mazuri na ya haraka kutoka kwa jopo la madaktari wa Kilimanjaro Stars, hivyo matarajio yao atakuwa fiti hivi karibuni.

“Yondani anaendelea vizuri kwa sasa na baada ya Krismasi ataanza mazoezi mepesi kwa sababu hali yake imeimarika haraka tofauti na wengi walivyotarajia, hivyo anaweza kuungana na timu.


“Tangu arejee nchini kutoka Kenya nimekutana naye mara moja na kuona maendeleo yake, lakini hivi sasa tumekuwa tukiwasiliana tu kwa simu akiwa kwao Mwanza alipoenda kupumzika mpaka hapo atakapoungana na wenzake Desemba 28,” alisema Bavu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic