December 15, 2017



Kikosi cha Zanzibar, Zanzibar Heroes, imetinga fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Uganda mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Moi, Kisumu, Kenya. 

Katika mchezo huo, Zanzibar ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 22 mfungaji akiwa Abdulaziz Makame lakini Uganda, The Cranes ilisawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Nsibambi Derrick.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi lakini dakika ya 57, Nsubuga Joseph alimchezea rafu Ibrahim Ahmada na kuonyeshwa kadi nyekundu huku akisababisha penalti.
Penalti hiyo ilifungwa na Mohamed Issa ‘Banka’ na kuipa Zanzibar bao la pili lililodumu hadi mwisho wa mchezo ambapo Zanzibar ilishinda mabao 2-1.

Kutokana na matokeo hayo Zanzibar inatarajiwa kucheza fainali na Kenya, Harambee Stars kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos, Kenya.

Katika nusu fainali, Kenya iliifunga Burundi bao 1-0. 

1 COMMENTS:

  1. mchezo uliochezwa leo na sio jana pia fainali kesho kutwa jumapili na sio kesho jumapili halafu stori umeandika leo ijumaa haileti maana.kuwa makini kama mwandishi wa michezo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic