Kikosi cha Zanzibar, Zanzibar Heroes, imetinga fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Uganda mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Moi, Kisumu, Kenya.
Katika mchezo huo, Zanzibar ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 22 mfungaji akiwa Abdulaziz Makame lakini Uganda, The Cranes ilisawazisha dakika ya 28 kupitia kwa Nsibambi Derrick.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi lakini dakika ya 57, Nsubuga Joseph alimchezea rafu Ibrahim Ahmada na kuonyeshwa kadi nyekundu huku akisababisha penalti.
Penalti hiyo ilifungwa na Mohamed Issa ‘Banka’ na kuipa Zanzibar bao la pili lililodumu hadi mwisho wa mchezo ambapo Zanzibar ilishinda mabao 2-1.
Kutokana na matokeo hayo Zanzibar inatarajiwa kucheza fainali na Kenya, Harambee Stars kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos, Kenya.
Katika nusu fainali, Kenya iliifunga Burundi bao 1-0.
Saleh Jembe mechi imechezwa Leo na siyo Jana kama unavyotanabaisha. Tafadhari tuombe radhi mashabiki na followers Wa blog hii.
ReplyDeleteWatanzania Bara wazembe kule Zanzibar hata league yenyewe ya mashaka lakini Zanzibar heroes wameshinda karibu kila mechi challenge cup kule kenya. Mtu huwezi kuitwa HERO au SHUJAA au STAR yaani nyota kuna mtu anaifikia nyota? alafu ukakubali kudhalilika kimdhaha mdhaha tu kama walivyofanya kiKilimanjaro stars nadhani vijana hawaijui thamani ya kupigania na kuliwakilisha taifa. Ningekuwa na mamlaka hao timu nzima ya Kilimanjaro wangefikia JKT angalau wiki mbili kujifunza uzalendo kidogo. Timu ya Taifa hasa ya mpira wa miguu ni kipimo tosha cha kujua au kupima uzalendo wa vijana kwa nchi yao. Huku Tanzania Bara kwenye mbwembwe za kila aina na league inayotambulika wameshindwa kushinda angalau mechi moja. Kwa kweli tuondoe siasa za chama cha mpira Tanzania Bara wakati wa kuzungumza ukweli umefika. Tanzania Bara kuna tatizo tena kubwa katika kusimamia maendeleo ya mpira. Kama tatizo sio chama cha mpira basi itakuwa makocha. Kama makocha sio tatizo basi wachezaji itakuwa tatizo. Kama wachezaji sio tatizo basi serikali kupitia wizara husika inayoshughulikia michezo ni tatizo. Hizi ni zama za ukweli na hii ni kauli thabiti ya Muheshimiwa raisi mpendwa Magufuli yakwamba msema kweli siku zote ni kipenzi cha Mungu. Hata ukimsikiliza na kumtizama katika hutuba zake wakati mwengine kama mtanzania wa kawaida unaingia uoga wakati anaposemea uovu zidi ya viongozi husika wakiwa mbele yao. Sasa unaposikia viongozi wa TFF na baadhi ya watu wanamumunya kwa kutoa vijisababu visivyokuwa na mshiko juu ya kuboronga kwa timu ya Taifa miaka nenda miaka rudi kwa kweli inakera. Bila kukubali kukosa na kukubali kukosolewa huwezi kujikosowa mwenyewe na huo ndio mwanzo wa kufulia hadi kuzimu. Najua kuna watu wana mawazo ya kisiasa yanapokuja malumbamo kati ya uwezo wa kimpira kati ya Zanzibar na Tz Bara huo ni upumbavu na kasumba za baadhi ya watu wanaotaka kutumia michezo kufikisha malengo yao ya kisiasa kupitia michezo kitu ambacho hata FIFA ni haramu kabisa na inakemea kwa nguvu zake zote. Lakini ukweli ni kwamba Zanzibar pia wana hoja ya msingi labda wanacheleweshewa maendeleo yao ya kweli ya mpira wanayoyatamani kimataifa kuyafikia kutokana na kuwa chini ya uongozi mbovu wa mpira Tanzania. Pengine ZFA na Zanzibar ingekuwa na uwakilishi wake binafsi ingetusaidia kujua ukweli halisi nani mzembe. Hata China na Taiwani ni nchi moja licha ya kuwepo msuguano wa kisiasa na nafikiri uwakilishi tofauti katika michezo kwa kitambulisho cha Chinese Taipei na Chinese Mainland. Wakati wa kuacha kuendesha shughuli zetu kwa mazoea yale ya kiuzembe uzembe tukitarajia kesho itakuja tena umepitwa na wakati. Tupambane na kufanya kazi kana kama nafasi tulioipata ni hadimu na vigumu kuipata tena katika maisha yetu.
ReplyDelete