January 15, 2018



Mmoja wa wanachama wakongwe wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa ataendelea kupinga suala la ukodishwaji wa klabu hiyo hadi atakapoingia kaburini na kudai kuwa wanachama waache kumsakama kwa kuwa Serikali ndivyo ilivyoamua.

Hivi karibuni Klabu ya Yanga ilitangaza kuanza mchakato wa mabadiliko kama ilivyo kwa watani wao Simba ambao wamemkabidhi timu Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa ajili ya kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu kwa njia ya hisa.

Akilimali amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa miongoni mwa wanachama ambao wanapinga mabadiliko ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limekuwa likiwachukiza baadhi ya wanachama.

Akilimali alisema kuwa, amekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa Yanga kutokana na kupinga suala la Yanga kumilikiwa na mtu mmoja na kudai kuwa ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoingia kaburini.

“Nimekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi, ni kutokana na kukataa katu suala la Yanga kumilikishwa mtu mmoja hilo haliwezekani na nitapinga hadi naingia kaburini.

“Nipo tayari uanzishwe mfumo wa kampuni kama inaavyotajwa katika katiba ya Yanga ibara ya 56 ambayo inasema Yanga itaanzisha kampuni ya umma ambapo wanachama wanamiliki hisa asilimia 51 na wanahisa asilimia 41.

“Lakini kwa kuwa nilikataa ndiyo naambiwa napinga mabadiliko, Yanga haikodishwi kama masufuria na kwa bahati nzuri serikali ikatusikiliza sisi watu wachache tuliopinga ukodishwaji ndipo wanaposema kuwa mimi napinga maendeleo.


“Mimi nahitaji maendeleo ya Yanga hadi kiama lakini utaratibu ufuatwe sio kumpa mtu mmoja, kwa kuwa viongozi wangu walitaka kukodisha na mimi pamoja na serikali kupinga, ndiyo wameniambia mimi napinga maendeleo, jambo hilo si sawa,” alisema Akilimali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic