January 24, 2018


Azam FC ilishaonja raha ya kileleni. Inaweza kurejea tena kama itaifunga Yanga katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Jumamosi.



Lakini Yanga wenye pointi 25 katika nafasi ya tatu, inataka kushinda na kuongeza pointi tatu pia. Azam FC wako katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 30 na vinara Simba wana 32.

Ofisa habari wa klabu ya Azam FC, Jafari Iddi maganga mapema leo amealika kikao cha waandishi wa habari kwa lengo la kuelezea namna klabu hiyo ilivyojipanga kuwavaa mabingwa wa tetezi wa kombe la Ligi Kuu Bara, katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye kikao hicho Maganga amesema kwamba, wanawakribisha sana Yanga kwenye uwanja wao kwani Jumamosi itakuwa ni siku ya kihistori kwa klabu hizo kwani itakuwa ni siku ya kwanza kucheza kwenye mchezo wa ligi ndani ya uwanja huo.

“Hadi sasa ratiba ya mchezo wetu dhidi ya Yanga inaonyesha utakuwa saa 1:00 usiku kwa mujibu wa ratiba ya TFF.

"Kama kutakuwa na mabadiliko ya aina yoyote ile tutawafahamisha maana kwenye mchezo wetu na Simba lilitokea badiliko la muda hivyo hata katika mchezo huu tuna wasiwasi lolote linaweza kutokea hivyo tutawafahamisha mapema iwezekanavyo.

“Mbali na  hilo nitumie muda huu kuwafahamisha kuwa timu yetu ipo safi na wachezaji wote wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo muhimu, kwani kila mmoja atakubaliana nami kuwa Yanga ni timu kubwa na tunaiheshimu hivyo tunajiandaa iwezekanavyo ili tuweze kupata pointi tatu mbele yao,” alisema Maganga. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic