January 24, 2018



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia amepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Kocha msaidizi wa Mwadui FC Jumanne Ntambi kilichotokea usiku wa kuamkia leo huko Shinyanga.

Rais Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia ya kocha huyo ,timu ya Mwadui FC,wanafamilia wa Mpira wa Miguu,ndugu ,jamaa na marafiki.

“Kifo cha Kocha Ntambi kimenishtua sana na kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wafiwa nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kumpoteza mpendwa wao,hakika alikuwa kocha aliyejitahidi kuibua vipaji na amekuwa na mchango mkubwa katika mpira wa miguu ambao bado alikuwa anautumikia mpaka kifo chake.” Alisema Rais Karia.

Kocha Ntambi hakuweza kuhudhuria mazoezi ya Mwadui yaliyofanyika jana kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu badala yake alifika mazoezini mwishoni kabla ya usiku mauti kumkuta akiwa nyumbani kwake,Mungu ailaze roho ya marehemu Ntambi mahala pema peponi,Amina.

Enzi za uhai wake Ntambi aliwahi kufundisha timu za Kahama United ya Shinyanga,Mlale JKT ya Ruvuma,Panone ya Kilimanjaro,Timu ya mkoa wa Shinyanga Igembe Nsabo na mpaka mauti yanamkuta alikuwa akiifundisha Mwadui ya Shinyanga akiwa kocha msaidizi.

Wakati huohuo Rais Karia pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa golikipa wa zamani wa Yanga na Simba Ismail Suma aliyefariki nchini Burundi.

Rais Karia ametoa pole kwa wafiwa kufuatia msiba huo wa Suma aliyefariki kwa maradhi ya ini na figo.


Suma wakati wa uhai wake mbali na kuvitumikia vilabu vya Simba na Yanga pia amewahi kuvitumikia vilabu vya Kariakoo United ya Lindi na African Lyon ya Dar Es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic