Azam FC imeitwanga Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi.
Mechi hiyo imeisha hivi punde kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Iddi Kipwagile alifunga bao katika dakika ya 59 akipokea pasi ya Frank Domayo aliyekuwa ameingia dakika ya 52.
Mechi ilikuwa nzuri na Simba ilionyesha soka safi, huku wachezaji wake wakipoteza pasi nyingi za wazi.
Hata hivyo, ukuta wa Azam FC ulioongozwa na Aggrey Morris ulikuwa imara kuzima mashambulizi ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment