January 6, 2018



Beki mwenye wa kulia wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy amewaziba midomo wale wanaomkejeli kuwa amebahatisha bao lake kwa kutamka kuwa, “Tulieni mtanikubali wenyewe.”

Kauli hiyo, ameitoa mara baada ya kuifungia Yanga bao pekee na la ushindi katika dakika 90 ya mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya JKU akipokea pasi ya Pius Buswita.

Beki huyo, tangu ametua Yanga katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara kikosi cha kwanza kutokana na ushindani anaoupata kutoka kwa Juma Abdul.

 Kessy alisema ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao kama beki anayetokea pembeni, lakini tatizo kubwa ni nafasi katika timu.

Kessy alisema, kama akiendelea kucheza mechi mfululizo anaamini atajijengea hali ya kujiamini na kuzoea na kufunga mabao katika mechi zijazo za Kombe la Mpinduzi na Ligi Kuu Bara.

“Lile bao nililolifunga limetokana na uwezo binafsi, kwani niliamua kukatisha katikati ya msitu wa mabeki kabla ya kumpasia Buswita aliyenirejeshea mpira kwa kisigino kabla ya mimi kufunga bao hilo.


“Nilitumia ujasiri huo baada ya kuona wapinzani wetu hawatoki golini muda wote wanalinda goli lao wakitaka suluhu wakati sisi tunataka pointi tatu, hivyo nikaona nilazimishe kwa kupasua katikati ya mabeki wao,” alisema Kessy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic