Kocha wa Simba, Irambona Masoud Djuma amesema kikosi chake kilicheza vizuri lakini hakikufanikiwa kufunga.
Djuma raia wa Burundi amesema kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC ni sehemu ya kile ambacho wanajifunza na lazima watakifanyia kazi.
Kocha huyo amesema: “Tulicheza vizuri na tulistahili kushinda, lakini hatukufanya hivyo na hii ni sehemu ya mafunzo ya mpira.
“Nafasi ya kuyafanyia kazi matatizo yetu yatakuwa dhidi ya URA, haitakuwa mechi rahisi. Watuunge mkono na sisi tutapambana uwanjani kurekebisha.”
Simba ilipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana.
Nimewaangalia simba wanacheza vizuri. Wanamiliki mpira. Wanatengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini bado wanakosa mtu au mtubukizaji mpira golini makini. John Boko kana kwamba anakosa jinsi ya kujiamini fulani kulingana na nafasi anazopoteza kufunga anatakiwa kutulia zaidi. Bila ya kupepesa Simba wanahitaji aidha kuwaeleza washambuliaji wao kujirekebisha kwa kuzitumia nafasi wanazozipata kwa kufunga au wataendelea kufukuza makocha. Tatizo la kutolewa kwenye FA na Green warriors ni tatizo lilojitokeza kwenye game ya mwenge. Halikadhalika kwenye mechi ya Azam. Nafasi nyingi zinatengenezwa za kufunga lakini umaliziaji mbovu. Kona 11 kati ya Azam hakuna hata moja ilizozaa matunda ni tatizo na kocha anatakiwa kuangalia suala hili. Na ndio maana timu zetu tunakutana warabu wanatuliza kila siku kwao wao kona ni penalt. Huwezi kuwapa kona tatu bila ya kukuadhibu na nadhani wanafahamu mapungufu yetu. Najiuliza kama muzamiri Yasini angeweza kubadishiwa majukumu kutoka kiungo hadi sentafowadi? Nadhani ni kijana mwenye shabaha ya magoli hata kujiamini zaidi anapokuwa na mpira. Mchezaji ambae anaweza kuwa na madhara makubwa anapokuwa kwenye eneo la hatari la mpinzani.
ReplyDeletesimba bado sana
ReplyDelete