Droo ya raundi ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inachezeshwa kesho Januari 5, 2018 ikishirikisha timu 32.
Raundi hiyo ya Tatu itahusisha timu nne(4) za mabingwa wa mikoa timu tatu(3) za Ligi Daraja la Pili,timu Kumi na Mbili (12) za Ligi Daraja la Kwanza na timu 13 za Ligi Kuu.
Hatua hiyo ya raundi ya tatu inabakiza timu Kumi na Sita(16) zitakazopambana kwenye hatua inayofuata.
Timu zitakazochezeshwa kwenye Droo ya hapo kesho ambayo itarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Azam ni pamoja na Buseresere ya Geita,Majimaji Rangers ya Lindi,Shupavu FC ya Morogoro na KariakooFC ya Lindi zote kutoka Ligi ya Mabingwa wa mikoa.
Nyingine zinazotoka Ligi Daraja la Pili ni Green Warriors ya Dar es Salaam,Ihefu FC ya Mbeya na Burkina FC ya Morogoro.
Zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo kutoka Ligi Daraja la Kwanza ni Toto Africans ya Mwanza,KMC ya Dar es Salaam,Friends Rangers ya Dar es Salaam,Biashara ya Mara,Polisi Dar ya Dar es Salaam,Polisi Tanzania ya Kilimanjaro,,Rhino Rangers ya Tabora,JKT Oljoro ya Arusha,Pamba FC ya Mwanza na Dodoma FC ya Dodoma.
Timu za Ligi Kuu zilioingia hatua hiyo ya raundi ya tatu ni Azam FC,Yanga(Dar es Salaam),Mtibwa Sugar ya Morogoro,Mbao FC ya Mwanza,Majimaji ya Songea,Kagera Sugar ya Kagera,Mwadui,Stand United (Shinyanga),Ruvu Shooting ya Pwani,Njombe Mji ya Njombe,Singida United ya Singida,Ndanda ya Mtwara na Tanzania Prisons ya Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment