January 4, 2018





Muda mfupi baada ya kutua Tanzania akitokea Morocco, kiungo wa Taifa Stars na Klabu ya Diffaa Al Jadida, Simon Msuva, alihudhuria msiba wa mama yake mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy, Uba Ally.

Mama yake Sure Boy ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia leo Alhamisi, alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo ambapo amezikwa leo jioni katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.


Sure Boy amesema: “Mama alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo, ugonjwa huo ndiyo chanzo cha kifo chake.”


Mbali na Msuva, pia Himid Mao na Aggrey Morris ambao wanacheza Azam FC, nao walihudhuria mazishi hayo pamoja na wadau wengine wa soka.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic