January 8, 2018


Beki wa kikosi cha  VfB Eppingen cha Ujerumani, Mtanzania Emily Mugeta ameanza mazoezi ya gym.

Mugeta ameanza mazoezi baada ya kukaa nje ya uwanja tokea Aprili, mwaka jana alipoumia.

Mugeta aliyewahi kukipiga Simba na Polisi Morogoro aliumia siku chache baada ya kutangazwa kwenye kikosi bora cha mwezi cha Ligi Daraja la Tano nchini Ujerumani.

Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka nchini Ujerumani, Mugeta amesema tayari ameruhusiwa kuanza mazoezi mepesi.

“Daktari kaniruhusu kuanza mazoezi ya gym. Itakuwa ni tayaratibu halafu ninatwenda naongeza kasi kutokana na maelekezo yake.


“Haukuwa wakati mzuri kwa kuwa nimekaa nje kwa miezi sita naa kwa sasa,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic