January 4, 2018





Hofu ya Simba na Yanga kwamba wanaweza kumkosa mdhamini sasa imetoewa.

Maan Kampuni ya kubashiri michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania imezitoa hofu klabu za Simba, Yanga na Singida United ya kuendelea kuzidhamini kama kawaida.

Hiyo, ikiwa ni moja tangu kampuni hiyo kusitisha udhamini wake kutokana na uamuzi wa serikali ya Kenya kuongeza ushuru.


Klabu ambazo SportPesa inazidhamini za kutoka Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na Ligi ya Super 8.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba alisema kilichokea Kenya cha kusitisha mkataba wa kuendelea kuzidhamini klabu, hausiki kwa Simba, Yanga na Singida United.

Tarimba alisema, wao SportPesa wamepanga kuendelea na udhamini wa klabu hizo za hapa nchini tena kwa kuzidi kuziboresha zaidi siku za baadaye ili kuhakikisha klabu hizo zinapata mafanikio.
Aliongeza kuwa, tofauti na udhamini wa klabu hizo, pia wamepanga kudhamini Ligi Kuu Bara kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litatangaza tenda ya udhamini.

“Niziondoe hofu klabu za hapa nchini ambazo tumezidhamini za Simba, Yanga na Singida kuwa uamuzi tuliouchukua wa kusitisha udhamini kwa klabu za Kenya kuwa hauziusu klabu za hapa nchini.

“Hivyo, kama SportPesa tumepanga kuendelea kuzidhamini klabu hizo huku tukipanga kuendelea kuziboreshea zaidi udhamini kwa siku zijazo katika kuhakikisha tunaendeleza soka.

“Labda nimalizie kwa kusema kuwa, mwaka huu wa 2018 tumepanga uwe wa mafanikio zaidi katika kuhakikisha soka la nchini linapiga hatua hapa nchini,”alisema Tarimba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic