Jeshi la Polisi nchini jana asubuhi lilivamia Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kuzuia kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa matawi wa klabu hiyo ulipangwa ufanyike.
Tukio hilo la aina yake lilitokea saa tatu asubuhi kwenye makao makuu ya klabu hiyo iliyopo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Temeke Kati na Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Bakili Makele, alisema kuwa mkutano ulizuiwa kufanyika na polisi kwa kile kilichodaiwa haukuwa na amani.
Makele alisema polisi hao waliofika kabla ya mkutano huo kufanyika walidai wamepata taarifa mkutano umepangwa kwa ajili ya uvunjwaji wa amani na kuwataka usimamishwe hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
Aliongeza kuwa, wao kikubwa katika mkutano huo walipanga kujadili masuala ya maendeleo na zaidi kuhusu ushiriki wa timu yao Kombe la Mapinduzi, Ligi Kuu Bara na hali yao ngumu ya kiuchumi.
“Polisi walifika kabla yetu, wakati tunaingia kwenye chumba cha mkutano, jeshi hilo la polisi likatuzuia kufanya mkutano likidai kuwa mkutano huo umeandaliwa kwa ajili ya uvunjaji wa amani.
“Taarifa hizo zilitushtua kiukweli, lakini tunashukuru sisi viongozi wa matawi na jeshi hilo la polisi tulifikia muafaka mzuri wa kukubali mkutano huo uahirishwe hadi pale upepelezi utakapofanyika, lakini niseme kuwa mkutano wetu ulikuwa na amani,” alisema Makele.
Kuna kila dalili sasa Yanga tunafanyiwa hujuma wazi wazi na ina kera sana.
ReplyDeleteMimi sio shabiki wa Yanga, ila ninachoshangaa tu ni kuwa kwanini polisi wasingebaki kuulinda huo mkutano na wale waliosadikiwa kuwa wangefanya fujo wangechukuliwa maelezo baada ya mkutano! Nawaza tu kwa sauti. Ila pia tuupinge utamaduni wa watu kufanya fujo kwenye mpira wa miguu. Uhuni huu unataka kumea mizizi na kuonekena ndio utaratibu TZ!
Delete