January 15, 2018



Straika wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, ametoa kali ya aina yake kwa kusema kuwa haoni tofauti yake na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa kuwa wote wameshindwa kufunga mabao ya kutosha msimu huu na hajui ni kwa nini.

Mussa ambaye aliibuka mfungaji bora msimu uliopita kwa kufunga mabao sawa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simon Msuva, aliyetimkia Morocco, mpaka sasa amefanikiwa kufunga bao moja katika mechi alizocheza, akizidiwa mabao saba na kinara wa ufungaji katika ligi ya msimu huu, Mganda Emmanuel Okwi.

Mussa alisema kuwa kupitwa mabao katika ligi ya msimu huu, hakuwezi kumkatisha tamaa ya kuvunja rekodi yake kwa kuwa hata Ronaldo ameshindwa kufanya hivyo kwenye ligi ya Hispania msimu huu kwani amefunga mabao manne tu mpaka sasa.

“Kiukweli kwamba ligi ya msimu huu ni ngumu, ushindani umekuwa mkubwa, najaribu kupambana kuona naweza kufunga vipi lakini siwezi na sijui kwa nini, siyo kwamba nafurahia hali hii kwa sababu bado nataka kufikia rekodi yangu ya msimu uliopita.


"Unajua siku zote mshambuliaji anatakiwa afunge na kitu ambacho nataka kiendelee kwa upande wangu maana kwa sasa naona sioni tofauti yangu na Ronaldo kwani hata yeye amekuwa anashindwa kufunga mabao na kufikia rekodi yake ya msimu uliopita hivyo watu wajue siyo kwamba nafurahia hali hii," alisema Mussa.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic