Kung’olewa kwa Simba katika michuano ya Kombe la Mapunduzi baada ya kuchapwa bao 1-0, kumezua mjadala mpya kuhusiana na Kocha Joseph Omog.
Omog raia wa Cameroon, alifungashiwa virago vyake na uongozi wa Simba ambao ulitumia maneno matamu kusema wamekubaliana aondoke baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na Green Worries inayoshiriki ligi daraja la pili.
Lakini baada ya kipigo cha leo, mashabiki wameanza kuhoji kama ilikuwa sahihi kumuondoa Omog.
Baadhi ya mashabiki wa Simba na wa timu nyingine wameeleza kuwa Simba ilikurupuka kumuondoa kocha huyo.
Lakini wako waliosema tatizo kubwa ni wachezaji wenyewe ambao wameshindwa kujituma na kuonyesha wanataka kushinda.
Pia kuna mashabiki ambao wameelekeza lawama zao moja kwa moja kwa Kocha Irambona Masoud Djuma kwamba mfumo wake unaonekana kuwa mgumu na si imara katika ulinzi.
Kipigo hicho leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kimekuwa cha pili mfululizo kwa Simba.
Mechi iliyopita, Simba ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Azam FC na matumaini yao kuendelea ilikuwa leo dhidi ya URA.
Bao la URA lilipatikana dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili, Simba ilishindwa kupata angalau bao moja.
Ukizungumza kiushabiki na hasira kweli utasema sababu ya kuondoshwa simba mapinduzi ni kutokuwepo Omog lakini kiuhalisia na kifutball Omog ndie alieifungisha simba mapinduzi cup. Kiuhalisia kikosi cha simba bado ni ya Omog. Ni kocha alieifundisha simba tangu pre season tena nje ya nchi .Mimi bado nashindwa kufahamu au kuwafahamu wachezaji wa simba hasa wabongo kama kweli wanajielewa au majipu yanayosubiri kutumbuliwa? Sina nia ya kuwakashifu hapana bali kwa kumbu kumbu simba mwaka huu imejitahidi sana kuwatunza wachezaji wake. Ni club pekee nafikiri kwa East Africa kuweka kambi yao nje ya ukanda wetu huu. Na nadhani hakuna pahala bora kwa maandalizi ya timu miongoni mwa nchi bora Africa kama South Africa kuweka kambi ya maandalizi. Hata walipokwenda Zanzibar walipojiaandaa kucheza na yanga waliweka kambi katika hotel bora kabisa. Mishahara haisimbui tena simba lakini licha kuwepo lawama za kocha wachezaji hawawezi kukwepa lawama. Nilianagalia goli walilofungwa simba na URA ni upumbabu hata kuangalia. Yule Nyoni alitikisha kiguu kidogo imradi aonekane alijaribu kufanya kitu hakuonekana hata kujali . Yaani wanamuacha mtu anakwenda kufunga wakimshindikiza kwa macho kwa kweli inakera. Kwa sisi tunaoshi nje ya nchi na kuadopt life style ya maisha ya uwajibikaji wa kazi za huku ni rahisi kupata matatizo ya moyo unapoona kiwango duni cha uwajibikaji cha wachezaji wanaolipwa na kazi yao kama wa simba. La kushangaza zaidi utasikia hao vijana wana ndoto ya kucheza ulaya? Mashindano kama mapinduzi cup utayaona madogo lakini maskauti kutoka South Africa sehemu nyengine wapo pale Amani kuangalia vipaji na wengine kufuatilia wachezaji fulani ambao tayari wamo kwenye madaftari yao. Samata katokea mazembe kwenda ulaya lakini amini usiamini simba ndio inayobeba jina la Samata Tanzania. Simba sio club ya mchezaji wa kitanzania anaepata bahati kuichezea mwenye malengo kwenda kuzembea pale. Ni sehemu ya kwenda kuwa mtumwa wa kujituma kwa nguvu zako zote ili kujitangaza. Sio club ya mchezaji kwenda kujifanya muhimu pale. Ni sehemu ya mchezaji au kijana mwenye malengo kuonesha umuhimu wa kuichezea simba kwa lengo la kujiendeleza zaidi. Banda ni kijana mdogo lakini alifahamu umuhimu wa kuichezea simba. Hata hayo mashindano ya mapinduzi kama angekuwepo basi pangechimbika. Banda hakuwa anaichezea simba kama analazimishwa.Alikuwa yupo tayari kupigana au hata kupata kadi nyekundu kuhakikisha lango lao linakuwa salama. Banda alikuwa na malengo hata mazoezi yake yalikuwa si ya kawaida. Ukiwa mvivu na kasumba ya kutojituma simba basi utakapokwenda ndio itakuwa hivyo hivyo. Na ndio maana kujituma kwa Banda akiwa simba ndiko kunakombeba South Africa. Na si ajabu wasauzi kuwa na hamu ya kumpata Banda mwengine kutoka au Tanzania . Wachina wanafomula inayosema unatakiwa kujituma zaidi mazoezini kujajirahishia kazi vitani. Kuwepo club ya simba au yanga kwa kijana mwenye malengo ya kusonga mbele ni sawa na kuwepo kwenye uwanja wa mazoezi kwa ajili ya vita ya kujitafutia mafanikio zaidi.
ReplyDelete