January 23, 2018


Gumzo kubwa limezuka mitandaoni, wadau mbalimbali wa mchezo wa soka wakijadili kuhusiana na beki wa Kagera Sugar, Juma Nyosso.

Wengi wanajadili kuhusiana na tabia zake lakini wengine wakihoji shabiki aliyepigwa na Nyosso kamaalikuwa sahihi.

Nyossoa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kutokana na tuhuma za kumshambulia kwa ngumi shabiki hadi akazirai.

Taarifa zinaeleza, Nyosso alimshambulia shabiki huyo mara tu baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Kagera na Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba na wageni wakashinda kwa mabao 2-0.

Wengi wawanaojadili wamekuwa wakisisitiza tabia mbaya za kibabe za Nyosso zinapaswa kukomeshwa.

Lakini wengine nao wamekuwa wakihoji kama shabiki huyo alikuwa sahihi kumtukana Nyosso na inaelezwa alimsogelea hadi karibu akitoa maneno ya kashfa.

Mjadala huo unaonekana kuelemea kwa Nyosso kwa kuwa kuna mifano ya kufanya vitendo vya kihuni uwanjani.


Lakini wako wanaohoji pia kuhusiana na shabiki ambaye anamkasirisha mtu aliyepoteza mchezo lakini kwa kumuambia maneno ya kashfa kuwa adhabu yake ni ipi hasa?

1 COMMENTS:

  1. TUKIMEE LAKINI LAZIMA TUWE NA HOJA....:
    Uwe uliingia vipi uwanjani...nawe Manara uliingia vipi uwanjani..Unaingia kama nani uwanjani???je kama huyo mshabiki angeenda kumdhuru mchezaji..je nani angekuwa wa kulaumiwa. Mchezo wa mpira joto lake ni kali zaidi na hata siasa. Unaweza kumpiga hata baba ake au hata kumtukana kwa sababu ya mpira wa miguu. Watu wengi tunamshutumu Nyoso kwa sababu ya kihistoria. Lakini tunajiuliza wewe shabiki ulienda kufanya nini uwanjani tena ndani kabisa nafuu hata ingekuwa nje ya uwanja.

    Kingine ni uhuni unaozidi kutengenezwa na msemaji na si afisa habari wa Simba SC wa kufanya vitu vilivyo nje ya propfessional yake. Unaacha kazi ya kufanya unaenda kuleta mambo ya ajabu ndani ya uwanja na inawezekana hasira za Nyoso zilinzia pale walipokwaruzana na Manara. Nahisi sasa tunatakiwa kumchukulia hatua kali Manara kabla ya kitu chochote ili liwe funzo kwa Maafisa Habari wasio na weredi kama wa huyu jamaa. Haiwezekani ulete ugomvi kama vyombo vya habari vilivyoongea.

    Tatu,,,shida ya walinzi wetu wanaokuja uwanjani kufanya kazi wanakuja kuangalia mpira na si kufanya kazi waliyotumwa. Inawezekana tukaanzisha kundi maalum la kulinda Uwanja kama wenzetu wanavyofanya. Pale inapotokea vurugu basi watapewa askari taarifa ili wasije uwanjani kuangalia mpira. Angalia tukio hadi washabiki wanaingia uwanjani..unajiuliza wenyewe walikuwa wapi...???Angalia tukio kama la Patrick Evra alimpiga mchezaji..ni kwa sababu ya tatizo ya lugha chafu ya washabiki.

    Kwahiyo tusiangalie pande moja tuu..tuangalie kote. Tusimuhukumu Nyoso kwa historia pia tuangalie makosa yetu sisi watendaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic