January 4, 2018



MSUVA AKIWASILI LEO ASUBUHI KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE.


Mshambuliaji nyota wa Difaa al Jadida ya Morocco, Simon Msuva ametua nchini kwa ajili ya mapumziko na kusema atapambana hadi apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Msuva amesema viwango vya Tanzania katika Fifa ni sehemu ya kikwazo lakini hatakubali kushindwa.

“Naendelea kupambana ili nifikie ndoto yangu ya kucheza Ulaya, nataka kufika huko lakini viwango vyetu vya Fifa bado. Lakini nitaendelea kupambana,” alisema.

Alisema amerejea nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja na nusu na atautumia muda huo kuwa karibu na familia yake.


1 COMMENTS:

  1. Kwa hili la viwango vya FIFA kuwa duni kwa Tanzania kwa kweli lina kera na kukatisha tamaa kwa sababu watanzania wengi tumekuwa tukipiga kelele miaka nenda miaka rudi na sio kelele tu bali ni ushauri ambao kama wahusika hasa TTF wangekuwa wanajali Tanzania tusingekuwa hapa tulipo. Ukichukulia hali ya nchi hapo nyuma kabla ya Magufuli kuingia madarakani ni dhahiri yakwamba karibu asimia 95% au niseme bila ya kukumunya aslimia mia moja 100% ya taasisi za serikali na mamlaka mengine zilifanya kazi katika mazingira ya ulaghai,uzembe,wizi, ubinafsi nakadhalika nakadhalika. Hiyo TFF ndio usiseme ilioza kabisa na mpaka sasa kama watanzania hatujaona mabadiliko yeyote ya maana pale. Na amini kama si mabadiliko ya kisiasa Tanzania hivi tunavyozungumza malinzi bado angekuwa wanaendelea na madaraka yake ya uraisi wake wa TFF. Kwa hivyo utaona kikwete alijitahidi nasikia hata serikali yake ilichukua jukumu la kugharimia huduma kadhaa za TFF na kubwa zaidi ni kuchukua jukumu la kugharimia malipo ya kocha wa timu za Taifa lakini bila ya shaka yeyote kuna watu walikuwa wakijinufaisha wao wenyewe binafsi na jitihada hizo za kikwete . Na ndio maana karibu makocha wote wa timu ya Taifa waliajiriwa wakiwa chini ya viwango na sifa ya kufundisha timu ya Taifa. Na bila shaka yeyote wahusika walikuwa wakiwakilisha price tag hewa ya malipo kwa kikwete. Ukiwa na mwalimu alie chini ya kiwango kwa ajili ya kuwaanda wanafunzi kwenda kushindana kimataifa basi tunachotarajia ni aibu tu. Mimi naseama tena yakwamba bado sisi kama watanzania hatujafikia kumteua mtanzania kuwa kocha wa timu ya Taifa yakwenda kushindana na timu za Taifa za Egypt,Ghana,Nigeria na ndio maana timu yetu ya Taifa huishia kufungwa na Burundi. Kumteua mtanzania kuwa kocha wa timu ya Taifa ni siasa za kijinga na ni miongoni mwa hujuma tunazijitakia sisi wenyewe katika maendeleo ya mpira. Sio kwamba napinga bila ya point ya maana hapana. Watu wenye akili watakwambia mwalimu wa chekechea au elimu ya awali au kinder garden lazima awe na elimu ya degree kwa sababu ndie mtu atakaejenga msingi wa elimu wa maisha yote ya elimu ya mwanafunzi. Ikiwa Misri au Mexico au hata Morocco wanaajiri makocha wa kigeni kwa ajili ya timu yao ya taifa kweli sisi watanzania tuna wachezaji wa zamani waliokuwa na uwezo wa kisoka au hata elimu ya soka kuliko wao hata tukawaamini kuwapa timu ya taifa? Utaona yakwamba wenzetu wapo serious kwa kutambua kuwa mchezo wa soka sio kitu cha kuchukulia poa bali ni vita kwani kuna maslahi mapana zaidi kule sisi bado tumelala kwa hivyo poleni sana vijana wa kitanzania mnaokumbana na kizingiti cha kushuka thamani licha yakuwa uwezo mnao kutokana na kuwa kiwango chetu kwenye rank ya FIFA ni ya aibu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic