Kocha Mrundi wa Simba, Irambona Masoud Djuma, jana alikataa katakata kuhojiwa na kituo cha Taifa cha TBC.
Pamoja na TBC, Djuma alikataa kuzungumza na waandishi wote waliofika katika bandari ya Dar es Salaam wakati Simba ikirejea kutoka Zanzibar.
Pamoja na juhudi za waandishi kumsihi azungumze, Djuma alikataa katakata huku akisisitizwa kufanya hivyo na meneja wa Simba ambaye kwa sasa si mtu anayejulikana sana.
Badala yake, Djuma alikwenda hadi alipopanda gari na kuondoka katika eneo hilo.
Simba imeng’olewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mechi mbili mfululizo.
Simba ilifungwa bao 1-0 na Azam FC kabla ya kukutana na kipigo kama hicho kutoka kwa URA na kuvurumishwa nje ya Kombe la Mapinduzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment