January 13, 2018



Baada ya kutolewa katika Kombe la Mapinduzi, Kocha wa Singida United, Hans Pluijm amesema nguvu zote anazielekeza kwenye mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Singida United iliondolewa katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na Azan FC bao 1-0 Jumatano wiki hii kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Singida United inacheza na Simba Januari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru huku zote zikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu zitoke katika Kombe la Mapinduzi.

Pluijm alisema; “Kutolewa na Azam katika Kombe la Mapinduzi kumeharibu mipango yangu yote niliyojiwekea ya kuhakikisha tunachukua kombe hilo ili tutakaporejea katika ligi kuu morali iongezeke.”

Katika kurejesha morali ya timu, Pluijm amepanga kushinda mechi dhidi ya Simba ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.


 “Hatutaki kupoteza mechi hiyo ya Simba katika mechi yetu ya kwanza baada ya kutoka Mapinduzi, hivyo ni lazima tushinde ili morali ya wachezaji iongezeke,” alisema Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga na raia wa Uholanzi.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic