Timu ya Prisons imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Katika mchezo huo wa Mbeya Derby, halikuchezwa soka la ufundi kutokana na uwanja huo kujaa tope iliyosababishwa na mvua kubwa ilionyesha kabla ya mchezo huo ambapo Prison walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya nane kupitia kwa Salum Bosco.
Dakika ya 30, Mbeya City walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa John Kabanda kabla ya Prison kupata penalti kufuatia mshambuliaji wake, Mohamed Rashid kuangusha ndani ya eneo la 18 na na beki wa Mbeya City, Ally Lundenga.
Boa la tatu la Prison katika mchezo huo lilifungwa na Mohammed Rashid dakika ya 87 kwa kumalizia mpira uliomshinda kipa wa Mbeya City, Owen Chaima. Mbeya City walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Babu Ally ndani ya dakika saba za nyongeza baada ya tisini kumalizika.
Ndani ya mud huo wa nyongeza, beki wa Prisons, Nurdin Chona alipewa kadi nyekundu na mwamuzi wa kati, Israel Nkongo kufuatia kucheza rafu ya makusudi katika dakika ya 97.
0 COMMENTS:
Post a Comment