Kipa mkongwe wa Yanga, Beno Kakolanya ameendeleza mgomo baada ya kutoonekana mazoezini.
Kakolanya amekuwa katika madai ya fedha zake dhidi ya uongozi wa Yanga lakini hakuwa amelipwa naye akaamua kutoshiriki mazoezi.
Kumekuwa na taarifa nyingine zikieleza uongozi wa Yanga uliamua kumuweka kando baada ya kumuonyesha mgomo.
"Kweli uongozi nao uliona akae kando, aliambiwa arejee mazoezini lakini hakufanya hivyo. Ndiyo maana hata safari ya Zanzibar, Kabwili ndiye akawa kipa namba mbili," kilieleza chanzo.
Hata hivyo, rafiki wa karibu wa Kakolanya, yeye ameiambia SALEHJEMBE kwamba kipa huyo ndiye anayeshinikizwa kulipwa haki yake na viongozi hawamjibu vizuri jambo ambalo limemkasirisha.
Nafikili waandishi tuanze angalau kupata habari illiyo kamili na iliyo fanyiwa upembuzi yakinifu kuliko mambo ya nusunusu. Saleh sidhan kama wewe kutoka hapo Mwenge hadi kwenye makao makuu ya Yanga ni Mbali....si zaidi ya nusu saa au saa nzima kama hakuna foleni. Naamini unaweza kupata habari itayoweza kusaidia umma wa wapenda mpira haswa washabiki wa Yanga kujua ni nini kinachoendelea kati ya pande hizo mbili. Kuliko kutumia sijui mnawaita rafiki wa karibu...maana kuna wengine wanaandika "Na Muandishi Wetu"...embu fanya kitu cha busara. Mtafute Mkwasa au Sanga muulize nini mustakabali wa Golie huyo
ReplyDeleteNafikili waandishi tuanze angalau kupata habari illiyo kamili na iliyo fanyiwa upembuzi yakinifu kuliko mambo ya nusunusu. Saleh sidhan kama wewe kutoka hapo Mwenge hadi kwenye makao makuu ya Yanga ni Mbali....si zaidi ya nusu saa au saa nzima kama hakuna foleni. Naamini unaweza kupata habari itayoweza kusaidia umma wa wapenda mpira haswa washabiki wa Yanga kujua ni nini kinachoendelea kati ya pande hizo mbili. Kuliko kutumia sijui mnawaita rafiki wa karibu...maana kuna wengine wanaandika "Na Muandishi Wetu"...embu fanya kitu cha busara. Mtafute Mkwasa au Sanga muulize nini mustakabali wa Golie huyo
ReplyDelete