January 24, 2018

ABBAS TARIMBA



Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI maarufu zaidi ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa kwa sasa imezidi kupaa hasa katika anga za kijamii kutokana na namna ambavyo imekuwa ikijitanua zaidi kusaidia kukuza ajira za Watanzania.


SportPesa imekuwa ikizidi kupiga hatua na kupata umaarufu mkubwa nchini kote kutokana na mambo ya michezo lakini zawadi zake ambazo zimetolewa kupitia shindano lake la Shinda na SportPesa ambalo watu 100 watashinda Bajaj.
Bajaj ambazo zinatolewa na SportPesa ni zile za kisasa aina ya TVS King Deluxe, ambazo ni maarufu kwa ubora na uimara wake.

Pamoja na  gharama kubwa ya ununuzi wa Bajaj hizo, Sportpesa imeamua kutoa Bajaj kwa watu 100, maana yake ni ajira ya uhakika kwa Watanzania 100 ambao wamejishindia kwa kushiriki kubashiri na kampuni hiyo ambayo kwa sasa ni ya kimataifa.

Wakati SportPesa inapambana kuhakikisha Watanzania wanafaidika, watu wanaopenda njia ya mkato kimaisha wao wakaanzisha utapeli kwa kuanza kuwatapeli watu mbalimbali wakiwaambia watawasaidia kushinda Bajaj.



Watu hao wamekuwa wakiwatumia watu ujumbe kwamba wao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo ya SportPesa na watawasaidia kushinda jambo ambalo Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji, Abbas Tarimba anasema haliwezekani hata kidogo.

“Kwanza hakuna kitu kama hicho, mfanyakazi wa SportPesa hawezi kufanya jambo kama hilo kwa kuwa haliwezekani hata kidogo.

“Anayeweza kushinda ni yule ambaye anafuata taratibu zinazotakiwa, kujisajili na kushiriki kubashiri na baada ya hapo ni suala la kikompyuta. Hakuna mtu mwenye uwezo wa kumpendelea mtu kusaidia ashinde, hata mimi au kiongozi mwingine hawezi kufanya hivyo,” anasema katika mahojiano na SALEHJEMBE, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

“Unajua wale wanachofanya wanatafuta namna za watu kwa kujaribu hii na ile na wakikupata wanakueleza kwamba wanatokea SportPesa, tuma shilingi laki moja kama unataka kushinda, ukifanya hivyo imeliwa. Mwisho watu wamekuwa wakilalamika.

“Siku moja nilimpigia yule mtu anayepigia watu, nikamueleza aache mambo ya kizamani na kumueleza tutachukua hatua. Naona kama wameacha lakini niwaambie watu kuwa SportPesa ni kampuni makini, hakuna haja ya kutuma fedha usaidiwe kushinda. Badala yake cheza kwa kufuata utaratibu kupitia ile namba yetu ya 5888, kama una bahati, utafanikiwa na sasa tayari Bajaj 90 zimeshatoka, kumi zinasubiri watu,” anasisitiza.

Katika washindi walioibuka na Bajaj, kinachowafurahisha SportPesa ni kwamba, washindi wamepatikana karibia Tanzania nzima, jambo ambalo wanalichukulia ni kama mafanikio makubwa sana.


“Wachezaji wa SportPesa wameshinda Bajaj karibu kila sehemu ya Tanzania. Angalia ni kutoka Kusini hadi Kaskazini, Kanda ya Kati Magharibi na Mashariki. Watu wameshinda Mwanza, Newala, Rukwa, Tanga na kadhalika.

“Utaona kama Mwanza na Makambako tumekuwa na washindi wengi zaidi kwa kuwa kila baada ya mmoja kushinda katika eneo husika, watu wanamuomba awafundishe na idadi ya kucheza inakuwa kubwa mwisho washindi wanapatikana wengine.


“Awali watu walikuwa wakiona ni kama vile haiwezekani, sasa anaposhinda mtu ambaye wanamjua, halafu kweli wanamuona ana Bajaj na awali hakuwa na uwezo wa kununua akiendelea na maisha yake ya biashara, basi wanaona ni kweli nao wanaingia kushiriki.”

Tarimba anasema wao wana kitengo maalum kwa ajili ya uendeshaji ambacho kinaongozwa na yeye ambaye ni mtaalamu wa masuala ya bahati nasibu.


“Watu ni watalaamu na wanaijua hii kazi. Ndiyo maana hauwezi kusikia kuna malalamiko kuhusiana nasi kwa kuwa hivi vinakwenda kwa utaratibu sahihi ambao unakuwa msaada mkubwa na hakuna mambo ya ujanja,” anasisitiza.


Tarimba amesema kwa kuwa SportPesa ni kampuni ya kimataifa, wataendelea kufanya masuala yao kwa weledi wa juu na kikubwa walichopanga ni kuisaidia jamii ya Watanzania ikiwa ni sehemu ya kurudisha kidogo wanachokipata kwa jamii.

SportPesa pia inafanya shughuli zake katika nchi za Kenya, Afrika Kusini lakini Uingereza na kwingineko Ulaya kama vile Italia na kadhalika.

Tarimba amesema wanachotaka ni kuendelea kushirikiana na wanamichezo kwa kuwa ndiyo wateja wao lakini jamii hasa katika kuisaidia serikali katika utengenezaji wa ajira kama ambavyo vile watu 100 watafaidika na ajira ya kujiajili wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa.

Pamoja na hivyo, Tarimba amesisitiza, SportPesa itaendelea kuijali michezo ya Tanzania na tayari imetoa mfano kwa udhamini katika klabu za soka kubwa tatu.


“Kwenye michezo tuna nia nzuri sana, nafikiri ni suala la muda tu na watu wameanza kuona namna ambavyo tunajitahidi na tunashirikiana kwa karibu sana na serikali yetu kuhakikisha michezo,” anasema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic