NANI KATI YENU ANAWAJUA HAWA…
Kampuni ya Avance Media imetangaza majina ya vijana 50 wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2017.
Imewataja vijana hao kwa kufuata mtiririko kuanzia namba moja hadi 50 lakini inaonekana kuna mapungufu mengi wakati wa utafiti wao.
Wengi wanaoelezwa kuwa na ushawishi ni watu wanaojulikana na jamii finyu au ni wale ambao hawakufanya chochote kikubwa mwaka 2017.
Ingewezekana kusema angalau moja kwa moja na si mwaka fulani. Lakini wako wanaonekana ushawishi wao mdogo au umepungua nguvu katika upande fulani, mfano michezo lakini wamepewa nafasi za juu au kutajwa.
Jumanne Mtambalike, Evans Makundi, Carlos Ndosi, Saira Dewji, Rebeca Gyumi, Krantz Mwatepele, Edwin Bruno, Fayaz Valli, Jebra Kambole, John Paul Barretto, Ian Ferrao, Osse Sinare, Harun Elias na Hellen Dausen na WANAFANYA NINI?
Kusema mtu ni mwenye ushawishi mkubwa wakati asilimia 90 ya jamii haimjui kabisa ni sahihi? Nafikiri watu wanapaswa kusaidiwa.
Mfano angalia kama Mbwana Samatta ambaye ameshika namba moja, hata asiyependa mpira atakuwa anajua ni nani. Wengine watakuwa hawajulikani sana lakini wanaweza kuwa wanajulikana na wengi.
Sijajua hawa ni influential kwa namna gani, huenda wangetoa ufafanuzi kidogo. Huenda ni wahamasishajiwa makundi maalum na watu wao labda hivyo.
Lakini kweli Faraja Nyalandu ni influential zaidi ya Ali Kiba na Diamond? au Salim Kikeke?
Jacqeuline Mengi naye ni influential kuliko Millen Magese, Flaviana Matata au Hasheem Thabeet? JIULIZE tena kama Mrisho Ngassa ni influential kuliko Thomas Ulimwengu au Joti?
Wako naona kweli wana ushawishi lakini kweli walikuwa na ushawishi huo mwaka 2017 au wahusika wamejiwekea tu.
Shomari Kapombe bado ni influential kwa maana ipi kama ni mwaka 2017? Ngassa ni influential 2017?
Ninaamini wahusika waliofanya utafiti huu walikuwa na nia nzuri lakini watu waliowatuma kuufanya hawakuwa makini.
Very week article. No research, no right to speak. Hao uliwataja kua hawana influence unajua wako sekta gani? Unajua wamefikia watu wangapi? Sababu wewe na kikundi cha watu uliozoeana nao (your circle) hamuwafahamu haimaanishi watu wote hawawafahamu. Tatizo mnawajua WaTanzania wapenda ''Ubuyu'' tu ndio maana una amini lazima wawe kina Ali Kiba na Diamond pekee. Kaka unapotea credibility, wewe ni mwandishi wa habari, USIKURUPUKE. Fanya tafiti kabla ya kuandika. Wengine uliowataja kwamba hawana influence wametajwa mpaka na Forbes Magazine kwa influence yao kwenye jamii. But well, huo muda wa kusoma Forbes magazine utaupata wapi wakati source ya habari zako ni Instagram.
ReplyDeleteGood idea wrong treatment
ReplyDeleteUliyecoment hapo juu hujiamini vile vileusingejiweka anonymous kama unaamini na unachokisema, huyo aliyetajwa forbes ni nani acha ujinga forbes sio miungu sawa na Tanzania sio Dar, Mwanza na miji mikubwa unaposema influential person uwe umefikia zaidi ya watu asilimia 50,na sio mnaoendesha programs zenu kwa mamilioni kwa ticket mseme influential. Mbwana amefanya wachezaji mpira wakaze but tukaona kina Msuva hao wametoka leo useme Ngasa amempita Msuva tu kwa mwaka 2017 usituletee usomi usio na mashiko. Mnatafuta kick ila kwa research hii mmeikosa poleni sana tena sana. Jembe endelea kukosoa wanafikiri unasafiri na nje na kujifunza ni Instagram ila wajinga kama hawa ndio wakutie ndimu kuendelea kutoa habari zilizonyooka.
ReplyDelete