January 12, 2018Ingawa imekuwa ni siri sana lakini taarifa zinaeleza, Neymar anajiandaa kuvunja rekodi yake usajili ya pauni milioni 198 aliyoiweka wakati akitokea FC Barcelona kwenda PSG.

Gazeti maarufu la michezo la Marca la Hispania, limeeleza kuwa tayari kumekuwa na mazungumzo kati ya PSG na Madrid, mazungumzo ambayo yamemhusisha baba mzazi wa Neymar.

Kiasi fulani imekuwa ikionekana ni kama ni kitu kisichowezekana lakini ripoti kutoka ndani ya Real Madrid zinaeleza, klabu hiyo tajiri imetenga pauni milioni 357.

Kama Madrid itamsajili Neymar kwa kitita hicho, maana yake nahodha huyo wa timu ya taifa ya Brazil atakuwa amevunja rekodi yake mwenye ya usajili.

Pia kama ataivunja rekodi hiyo kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 357 kwenda Madrid, basi huenda ikachukua zaidi ya miaka mingine mitano hadi 10 kabla haijavunjwa.


Hii inatokana na namna ambavyo inaonekana Lionel Messi ameamua kumalizia mpira wake FC Barcelona lakini kwa Cristiano Ronaldo hata kama atahama Madrid, bado inaonekana itakuwa kazi nguvu kuifikia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV