January 13, 2018



Kesho Jumapili African Lyon itacheza na Friends Rangers katika mechi kali ya Ligi Daraja la Kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, hisia za watu wengi zipo katika mchezo huo.

Kocha wa Friends Rangers, Khalid Adam amesema wanajua African Lyon ni timu kubwa iliyowahi kucheza Ligi Kuu Bara, lakini watapambana kuifunga.


Ugumu wa mchezo huo ni mkubwa kwani katika Kundi A walilomo, African Lyon ipo nafasi ya pili na pointi 18 huku Friends Rangers ikiwa nafasi ya nne na pointi 16, kileleni yupo JKT Ruvu na pointi 25. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic