January 27, 2018



Yanga ikicheza na Azam FC leo Jumamosi, daktari wa zamani wa Taifa Stars, Sheck Mngazija ameionya Yanga kuhusu kumtumia Amissi Tambwe kutokana na kuumia goti kila mara ndani ya muda mfupi.

Tambwe, straika raia wa Burundi amecheza mechi tatu tu za Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa amekosa mechi 11 kutokana na majeraha ya goti la kulia.

Straika huyo aliyejiunga na Yanga msimu wa 2014/15 akitokea Simba, katika siku za hivi karibuni amekuwa akiumia goti kila wakati jambo linalomfanya kukosa mechi za timu yake.

Kutokana na hali hiyo, Mngazija ambaye ni mtaalamu wa afya za wanamichezo, amesema kuwa, Tambwe huwa haponi vizuri ndiyo maana amekuwa akiumia kila wakati.

Alisema hali hiyo inatokana na tabia yake ya kupenda kucheza soka kila wakati ili aweze kuwalidhisha viongozi wake pamoja na mashabiki pasipo kujali afya yake.

“Kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwashauri tu Yanga pamoja na yeye mwenyewe (Tambwe) kuhakikisha anapona kabisa ndipo arudi uwanjani vinginevyo atashindwa kucheza soka.


“Tatizo la goti siyo kitu cha kuchezea, watu wengi wameachana na soka kwa sababu ya goti, kwa hiyo uongozi wa Yanga pamoja na yeye mwenyewe wanapaswa kuwa makini na hilo,” alisema daktari huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Ushauri bora kabisa , Angalia Kapombe amepumzika muda mrefukujiuguza. Bado tunawahitaji wachezaji wetu jarini afya zenu kama daktari anavyoshauri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic