February 1, 2018


NA SALEH ALLY
Klabu ya klabu ya Singida United, imeamua kumsimamisha mchezaji wake, Papaa Kambale kwa muda usiojulikana.

Kambale alifanya vurugu katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons na baadaye akafanya hivyo katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Green Worriers.

Katika mechi hiyo alitolewa nje kwa kadi nyekundu jambo ambalo Singida United imeliona si sahihi.

Katika barua ya kumsimamisha Singida United imeeleza wazi kwamba imeona kuna upungufu na ukosefu wa umakini.

Moja kwa moja imekemea tabia hiyo ya Kambale ambaye ni mchezaji wa kimataifa ikieleza alitakiwa kuonyesha mfano bora badala ya alichofanya.

Binafsi naipongeza Singida United kwa uamuzi wa kiweledi, uamuzi sahihi katika muda sahihi baada ya kutokea kwa matukio mawili ya Kambale.

Kambale hawezi kuwa mkubwa kuliko Singida United, kama ingeuwa hivyo, basi yeye ndiyo angeiajiri Singida United na ingemtumikia yeye.

Uongozi wa Singida United, umefanya jambo la kiweledi na funzo kwa klabu nyingi za Tanzania ambazo uamuzi wao mwingi umekuwa ukijali zaidi ushabiki.

Viongozi wa Singida United wameamua kwa manufaa na heshima ya klabu yao na adhabu ya Kambale itawafanya wachezaji wengine waone wanafanya kazi na watu makini na wasio na mzaha.

Kambale ameadhibiwa na Singida United katika kipindi inamtegemea lakini imemuonyesha inataka jambo gani. Inataka soka na nidhamu na si longolongo na ubondia au maneno mengi mdomoni.

Wale ambao mmekuwa mkiwafanya wachezaji wenu wajione miungu watu, leo bila ya kiingilio wala nauli, Singida United wamewapa somo la bure kabisa.


1 COMMENTS:

  1. Uongozi safi kabisa Singida United. Sio wenzangu wa Kagera Sugar wanatetea maovu ya wachezaji wake hiyo sio sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic