February 26, 2018


Na George Mganga

Kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC jioni ya leo, Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Nicolous Gyan leo amefunga bao lake la kwanza.

Gyan ambaye alisajiliwa na Simba na kuanza kuichezea msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amefunga goli hilo katika dakika za mwisho za mchezo.

Baada ya beki Erasto Nyoni kufunga bao la 4, Gyan ambaye hajawahi kufunga hata katika mechi za kirafiki, alicheka na nyavu katika dakika ya 86.

Goli hilo lilikuwa muhimu kwa Simba kwani lilifanya idadi ya mabao kuongezeka na kufika matano.

1 COMMENTS:

  1. Mwandishi ni kweli Gyan hajawahi kufunga hata mechi ya kirafik???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic