February 26, 2018



Na George Mganga

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ulipangwa kuzikutanisha Yanga na Mtibwa umeahirishwa ili kuipa nafasi Yanga kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo ambao ulipaswa kupigwa mapema baada ya Yanga kucheza na Ndanda FC mkoani Mtwara, sasa utapangiwa tarehe nyingine hapo baadaye.

Yanga itacheza mechi yake na Ndanda February 28 2018, na kisha baada ya hapo itapata muda wa kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Mchezo huo dhidi ya Rollers, utachezwa March 6 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. Jamani acheni mambo yaleyale ya kupanga mechi baadae. Kwanini? Mbona mechi ya Simba na Stand United ilipangwa ichezwe tarehe 4 Machi umebadilishwa sasa imepangwa kuchezwa tarehe 2 Machi. Huu mchezo wa Yanga na Mtibwa ulikuwa uchezwe mapema Machi sasa unaahirishwa bila kuwekewa tarehe nyingine. Tusifanye hivyo . Pangeni tarehe na itangazwe wote tujue.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic