Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya
Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi
18,2018 Madagascar.
Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally
Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli
Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce
Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed
Msafiri Mgoyi, ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club
Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini
utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa
kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec
Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo
Ndola.
0 COMMENTS:
Post a Comment