Kamati ya Maadili ya TFF ilIyokutana Februari 3,
2018 na Februari 17,2018, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo mengine
yaliyojadiliwa pia ilipitia na kutoa hukumu ya tuhuma za kutoa taarifa zisizo
sahihi na kughushi leseni za usajili zilizowakabili watuhumiwa mbalimbali
walioletwa mbele yake.
Tuhuma hizo zilitokana na mechi namba
26 kundi A Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika 29 Oktoba 2017 kati ya Mvuvumwa
FC na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo timu ya Mvuvumwa FC
iliwachezesha wachezaji watano (5) ambao ni Elias Costa Elias (aliyevaa jezi
namba 5), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdala Dunia (jezi
namba 1), Doto Justine Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi
namba 8).
Viongozi
waliotuhumiwa ni Dr. Yared Fubusa (Mwenyekiti na Mmiliki wa timu),
Ramadhani Kimilomilo (Katibu wa Mvuvumwa FC), Joseph Kanakamfumu (Kocha
na Mratibu wa timu), na Yusuph Makoya (Mratibu wa timu). Wachezaji wa
Mvuvumwa FC waliofunguliwa mashtaka ni Elias Costa
Elias, Lukwesa Joseph
Kanakamfumu, Dunia Abdala
Dunia, Doto Justine
Kana na Mwarami Abdala
Mwaram.Kushiriki mechi namba 26 kundi A Ligi daraja la kwanza iliyofanyika 29 Oktoba 2017 kati ya Mvuvumwa FC na Friends Rangers, huku wakijua usajili wao haujakamilika ikiwa ni kinyume na kifungu 37(14) cha Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2013.
Kosa la pili ni Udanganyifu na kugushi leseni wakati wa usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
HUKUMU
Wachezaji
Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine
Kana, na Mwarami Abdala Mwarami
Kamati
haikuwakuta na hatia yoyote wachezaji hawa kwa vile walishiriki Mechi Na. 26
baada ya kupotoshwa na viongozi wao kwa kuaminishwa kuwa usajili wao
ulikamilika na wakapewa sehemu ya fedha walizoahidiwa kwa ajili ya kusaini.
Vile vile wachezaji hawa hawahusiki na suala la usajili, hivyo hakukuwa na
uwezekano wa wao kugushi leseni.
Hata hivyo Kamati inawakumbusha wachezaji wote kuwa
makini wakati wa kufanya makubaliano na timu zao kwani mpira ni ajira kwao.
Suala kama hili linaweza kuwanyima fursa ya kukitumikia kipaji chao na
kuwasababishia matatizo ambayo yanaweza kuepukwa kwa wao kuwa makini. Endapo
wanakutana na vikwazo au kuhisi mazingira ya ubabaishaji ni vizuri waombe
ushauri na msaada TFF.
HUKUMU
- Ndg. Joseph Kanakamfumu – Kocha na Mratibu wa Mvuvumwa FCKamati imemtia hatiani kwa makosa yote mawili; Kutoa taarifa zisizo sahihi/udanganyifu ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na kifungu cha 41(12) ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2017 na kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.Katika kosa la kwanza, Ndg. Kanakamfumu, akiwa kocha wa Mvuvumwa FC aliwaorodhesha wachezaji Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami kushiriki Mechi Na. 26 huku akijua kuwa hawana leseni halali kutoka TFF. Wachezaji wote hao walitoka katika kituo (academy) anayoiendesha, hivyo ni dhahiri kuwa alijua alichokuwa anafanya.Katika kosa la pili, Ndg. Kanakamfumu aliamua kuwaongeza wachezaji hao baada ya kukabidhiwa timu kwa vile alifahamu uwezo wao na inaonekana alitumia uzoefu wake katika mpira wa miguu kupata leseni hizo za kugushi.Kwa makosa hayo, Kamati inamfungia Ndg. Joseph Kanakamfumu kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.
- Ndg. Ramadhani Kimilomilo – Katibu wa Mvuvumwa FCKamati imemtia hatiani kwa kosa kushiriki kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.Ndg. Kimilomilo akiwa kama Mtendaji Mkuu wa Mvuvumwa FC alishindwa kusimamia timu yake ipasavyo na kusababisha ichezeshe wachezaji wasio na leseni. Aidha Ndg. Kimilomilo hakutoa taarifa TFF wala Bodi ya Ligi au kuchukuwa hatua zozote kwa Ndg. Joseph Kanakamfumu licha ya kukiri mbele ya Kamati kuwa wachezaji hao hawakuwemo katika orodha ya Mvuvumwa FC. Hii inamaanisha kuwa alishirikiana na viongozi wenzake kugushi leseni ili kuiongezea nguvu timu yake.Kwa makosa hayo, Kamati inamfungia Ndg. Ramadhani Kimilomilo kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.
- Dr. Yared Fubusa – Mwenyekiti na Mmiliki wa Mvuvumwa FCKamati imemtia hatiani kwa kosa la kushiriki kugushi leseni kipindi cha usajili kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.Dr. Yared Fubusa akiwa Mwenyekiti na Mmiliki wa Mvuvumwa FC amehusika kwa sehemu kubwa katika uendeshaji mbovu wa timu hali iliyosababisha matatizo mengi ikiwa suala la kugushi leseni za wachezaji Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami Abdala Dunia, Doto Justine Kana, na Mwarami Abdala Mwarami.Kwa mujibu wa maelezo ya Ndg. Joseph Kanakamfumu, kulikuwa na mawasiliano kati yake na Dr. Fubusa kuhusiana na uendeshaji wa timu. Hata suala la kuongeza wachezaji ili kuimarisha timu liliwezekana baada ya kupatikana fedha za kuwalipa kwa ajili ya kupata saini zao. Maelezo hayo yalithibitishwa na Ndg. Kimilomilo, Katibu wa Mvuvumwa FC. Kamati inaona kuwa Dr. Fubusa, ambaye alikuwa anatoa fedha za uendeshaji wa timu, alikuwa anapewa taarifa zote za matumizi yake. Aidha kama Mwenyekiti na Mmiliki alipaswa kujua kila kinachoendelea katika timu yake.Alipopewa taarifa ya wito wa kufika mbele ya Kamati ya Maadili, Dr. Fubusa alinukuliwa akisema kwa njia ya simu kuwa “TFF ni wapumbavu, mimi siwezi kuja huko. Kwanza mimi ndiyo mhanga”. Kauli hiyo ni ya dharau na ni kinyume na Kifungu cha 73(5) & (8) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.Kwa makosa hayo, Kamati inampa adhabu zifuatazo;
1. Kosa la kukaidi wito huku yeye akiwa mwanafamilia ya mpira wa miguu, Kamati inamfungia kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tatu (Sh.3,000,000.00). adhabu hii ni kwa mujibu wa 73(5) & (8)(a) cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013.
2. Kwa kosa la kusaidia kugushi leseni za wachezaji wa Mvuvumwa FC ili washiriki Mechi Na. 26, Kamati inamfungia kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano (5). Adhabu hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.Adhabu zote mbili atazitumikia kwa pamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment