Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limewapanga
waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho
Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7, 2018
Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka
akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi
Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa
Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka
Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17,
2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre
akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes
Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba
atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal
Salem Embaia.
0 COMMENTS:
Post a Comment