February 26, 2018


Na George Mganga

Michuano ya Kombe la Shirikisho iliweza kuendelea tena siku ya leo kwa mechi mbili kuchezwa kwenye viwanja tofauti.

Stand United ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani imeifunga Dodoma FC kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kusonga mbele.

Mechi nyingine ambayo imechezwa ni Kiluvya United ambayo ilipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons ya Mbeya.

Baada ya mechi hizo kukamilika, Tanzania Prisons na Stand United zimeweza kuingia nane bora ya mashindano hayo.

Timu zingine zilizoingia hatua ya 8 bora ukiachilia Tanzania Prisons na Stand United ni

Azam FC
Young Africans
Njombe Mji FC
JKT Tanzania
Mtibwa Sugar FC na
Singida United

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic