February 21, 2018



Mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa mpira barani Afrika na duniani kote katika UEFA Champions League, ni kati ya Chelsea dhidi ya FC. Barcelona ambayo imemalizika kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo huo ambao Barcelona walitawala zaidi haswa eneo la kati, ulishuhudiwa kwa Chelsea kucheza kwa mfumo wa kujilinda zaidi, huku Willian akipiga mikwaju miwili iliyogongwa mwamba.

Dakika ya 62 ya mchezo, Willian alianza kutikisa nyavu kwa shuti kali alilopiga karibu na usawa wa mita 18, huku Mlinda Mlango wa Barcelona, Ter Stegen akibaki mikono mitupu.

Makosa ambayo yalikuja kuigharimu Chelsea katika dakika ya 75, ni pasi fyongo iliyopigwa na beki wake, Andreas Christensen na kumfikia Andres Iniesta, ambaye alimtengenezea Messi na kupasia kambani mpira huku ubao ukibadilika na kusomeka 1-1.

Matokeo hayo sasa yanaipa faida Barcelona ya kuwa na bao la ugenini, ambapo mchezo wa marudiano utapigwa Camp Nou, Jumatano ya March 14 mwaka huu.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic