February 20, 2018






Mafarao wa Misri, Al Masry wameangukia pua baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Hata hivyo, Al Masry wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 wakiwa nyumbani Misri na sasa hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho, wanakutana na Simba.

Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.

Maana yake, Simba inakwenda kukutana na mlima mwingine raundi ya mapema tu baada ya kurejea katika michuano ya kimataifa.

Mechi ya kwanza itaanzia jijini Dar es Salaam, kabla ya Simba kufunga safari na kwenda Misri kumalizia ngwe hiyo inayotarajia kuwa ngumu.


Simba ina heshima kubwa kwa kuwa imewahi kuivua ubingwa na kuing’oa mashindano Zamalek ya Misri, timu kubwa ya pili na moja ya klabu maarufu barani Afrika.

1 COMMENTS:

  1. Hongera Simba. Anzeni sasa mazoezi kamilifu ya kuwafunga wamisri hao. Simba inao uwezo wa kuwafunga isipokuwa lazima iongeze umakini katika uchezaji wao. Wamisri wepesi hucheza kwa spidi. Simba lazima itumie vizuri nafasi za kufunga. Wachezaji wanatengeneza nafasi nyingi lakini zinapotea nyingi kwa kupunhua umakini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic