February 20, 2018




Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendamarie na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa idadi ya mabao 5-0.



Katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda kwa mabao 4-0.

Bao la leo la Simba lilifungwa na  Emmanuel Okwi, Simba ikiwa imekianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa.

Mechi hiyo ilikwenda mapumziko kwa sare ya bila bao huku Gendamarie wakipoteza nafasi moja ya kufunga na Simba wakipoteza tatu ikiwemo ya Okwi aliyekuwa nahodha katika mchezo wa leo.


1 COMMENTS:

  1. Hongera Simba. Anzeni mazoezi makali ya kukabiliana na Waarabu pamoja na kumaliza kazi ya Ligi kuu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic