February 28, 2018


Beki Salim Mbonde ameendelea kujifua na wenzake na kuonyesha matumaini mapya ya kurejea na kuboresha zaidi safu ya ulinzi ya Simba.


Beki huyo aliyekuwa majeruhi amekuwa akirejea taratibu na baadaye amejiunga na wenzake katika mazoezi.

Katika mazoezi ya Simba leo, Mbonde alikimbia taratibu peke yake kabla ya kuungana na wenzake na kuonyesha kuwa kweli anaanza kurejea.

Simba imeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na zile za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ambao ni vinara wa ligi kuu watacheza na Stand United katika mechi inayofuata na Shirikisho Afrika wanawasubiri Mafarao wa Al Masry.

Kikosi hicho kimejifua chini ya kocha wake, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa anayesaidia na Mrundi Masoud Djuma na raia wa Tunisia, Mohamed Habibi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic