Kiungo Haruna Niyonzima tayari ameanza matibabu ya mguu wake ambao umekuwa ukimsumbua.
Taarifa zinaeleza, Niyonzima ameanza matibabu hayo kwa kuchomwa sindano maalum na baada ya hapo atakuwa katika uangalizi maalum.
“Sindano hiyo ni maalum na madaktari watakuwa wakimfuatilia kwa uangalizi wao maalum,” kilieleza chanzo.
“Nimezungumza naye kwa kweli anaendelea vizuri na matumaini ni kuona anarejea haraka kabla ilivyokuwa inatarajiwa.”
Madaktari hao wa India wameshauri Niyonzima asifanyiwe upasuaji kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali.
Kiungo huyo nguli kutoka Rwanda hakupata nafasi ya kuonyesha cheche zake Simba aliyojiunga nayo akitokea Yanga baada ya kuumia mapema tu.
Hali hiyo imemfanya akae nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano sasa.
Hiyo picha gani inastua watu bila sababu?
ReplyDelete