February 21, 2018Na George Mganga

Klabu ya Mbao FC imeondolewa rasmi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho (FA Cup), baada ya kufungwa jumla ya matuta 6-5.

Katika mchezo huo uliokuwa wa hatua ya 16 bora, dakika 90 zilimalizika kwa matokeo ya bao 1-1, huku Njombe Mji wakianza kucheka na nyavu katika dakika ya 39 kipindi cha kwanza kupitia Ditram Nchimbi.

Mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Sabasaba jioni ya leo, ilidumu kwa dakika 45 za kwanza huku matokeo yakiwa ni 1-0, Njombe Mji wakiwa wanaongoza.

Said Said aliweza kuisawazishia Mbao FC katika dakika ya 79 na kuufanya mchezo umalizike matokeo yakiwa ni 1-1.

Hatua ya penati ilifuatia na Mbao FC ikaweza kuondolewa.

Ikumbukwe Mbao ndiyo walikuwa mabingwa namba 2 baada ya kufungwa na Simba katika fainali iliyochezwa mjini Dodoma mwaka jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV