February 21, 2018



Na George Mganga

Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gendarmarie Nationale FC, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho siku ya jana, Simba sasa itacheza na Al Masry SC March 6 2018.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya Simba kufikisha jumla ya mabao 5-0 katika Aggregate.



Simba ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuwakaribisha Al Masry hapa nchini, mchezo ukipigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Saalam.

Baada ya mechi hiyo, mchezo wa marudiano utachezwa March 16 2018 katika Uwanja wa Al Masry Club, utakaochezwa nchini Misri.

Masry wanakutana na Simba baada ya kuiondoa Gren Buffaloes kwa jumla ya mabao 5-2.

1 COMMENTS:

  1. Simba SC chonde chonde viongozi anzeni mazoezi na matayarisho ya nguvu mara moja kwa mchezo huo. Tunao uwezo wa kuwashinda. Mbinu wanazotumia ni kujilinda wanapokuja huku ugenini na tutapoenda kwao wanabadilika kuwa nyuki na vurugu zozote watafanya. Simba mnawajua sana warabu. Safari hii hapahapa nyumbani tuwabomoe kwelikweli goli 4 bila huruma. Tukienda kwao tunajua ushindi sio rahisi tutaenda kulinda ushindi wa nyumbani na kushambulia kwa kustukiza. Tunaweza .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic