ONYO LA MASAU BWIRE KWA WANAOIKEBEHI RUVU SHOOTING, HILI HAPA
Na George Mganga
Baada ya ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jana, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, ametoa onyo kwa wanaoidharau timu hiyo.
Bwire alitoa onyo hilo mapema jana baada ya mchezo kumalizika wakati akizungumza na ripota wa Saleh Jembe kuwa wale wote wanaodharau timu hiyo na walikuwa wanaipa nafasi ya kuteremka daraja, amewataka waondoe mawazo hayo.
"Niseme tu kwamba wale wote walikuwa wakiikebehi na kuidharau timu yetu, kisa kutofanya vizuri katika mechi za mwanzo, nawaomba waondoe mawazo hayo. Sasa hivi tuna mwendo mzuri na hakika tunayekutana naye mbele yetu ajipange'' alisema Bwire.
Ruvu Shooting sasa ipo katika nafasi ya 7 ya msimamo wa Ligi kwa kuwa na alama 23, chini ya Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 6 yenye alama 27








0 COMMENTS:
Post a Comment