February 22, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema anakijua kikosi cha Al Masry cha Misri, lakini akaonya.

Simba itakutana na Al Masry mwanzoni mwa mwezi Machi katika mechi ya Kombe la Shirikisho, timu zikiandia Dar es Salaam.

Lechantre raia wa Ufaransa amesema timu hiyo si ya kubeza, ngumu na inahitajika maandalizi ya kutosha.

Kocha kuyo amesema: “Hakuna kisichowezekana, tuna kikosi kizuri na tuna uwezo wa kuwatoa. Lakini haiwezi kuwa rahisi.

“Lazima tujiandae vizuri, tufanye kazi kwa uhakika na ninaamini tutafanya vizuri.”


Kocha huyo amewahi kufanya kazi nchini Tunisia na nchi nyingine mbalimbali za Ukanda wa Afrika Kaskazini na barani Asia.

1 COMMENTS:

  1. Hiyo ndio mechi kwa watanzania kuanza kufurahia michuano hii. Timu za Misri ngumu na wanjua kuucheza mpira. Simba pia inajua kuucheza mpira. Muhimu kujiandaa mapema na kwa wachezaji kujituma sana uwanjani. Tunaweza.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic