February 22, 2018



Wakati akiwa anaitumikia timu yake huko Shelisheli, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepatwa na msiba baada ya kufiwa na mwanaye.

Mwanaye ambaye alikuwa bado mchanga amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis.


Yanga ilipata sare ya mabao 1-1 na kusonga mbele huku Cannavaro akicheza kwa dakika 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic