Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja
waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani
Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana
utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana
akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi
namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland
Mangaluso Jabulani Langwenya
Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini
Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na
mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili
Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo
anatoka Africa Kusini Gay Makoena.
0 COMMENTS:
Post a Comment